Na Jacqueline Massano
Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) umewasimamisha wanafunzi 17
wa kitivo cha Elimu na Sanaa kwa muda usiojulikana kutokana na utovu wa
nidhamu.Barua hizo ambazo NIPASHE iliona nakala zake zilitolewa kwa wanafunzi hao juzi na kusainiwa na Mkuu wa Kitivo cha Elimu, Jonathan Kabigumila, ziliwataka kuondoka chuoni hapo ndani ya saa nne.
Baadhi ya wanafunzi waliosimamishwa ni Raban Seth, Bigambo Simon, Frank Sempombe, Daniel Mafuru, Fikiri Kalogi, Maryness Abdallah, Mary Philipo, Mjungu, Rafiki Lufunga, Nashon na Kanunga Christom.
Wakizungumza katika ofisi za NIPASHE mjini Dodoma jana, wanafunzi hao walisema kuwa wanashangaa kupewa barua za kusimamishwa zikiwa na makosa saba ambayo hawajayatenda.
Mmoja wa wanafunzi hao, Sempombe Frank, alisema katika barua yake aliyopewa ameelezwa kuwa ameharibu vifaa vya chuo na vya wanafunzi wenzake.
Alisema kosa lingine ni kuwa amewashawishi wanafunzi kugoma na kusababisha uongozi kupata na msongo wa mawazo kitu ambacho si kweli.
Daniel Mafuru, alisema aliitwa na mshauri wa wanachuo na kuulizwa kwa nini anafanya siasa chuoni hapo kitu ambacho anasema si kweli.
“Aliponiuliza hivyo, nikamwambia mimi sifanyi siasa chuoni kwa sababu sijawahi kuitisha mkutano wowote wa kisiasa chuoni hapa.
“Ndipo mkuu wa chuo wa kitivo cha elimu akaniuliza wewe ni mwanachama wa chama gani? kutokana na swali hilo sikuwa na jibu la kujibu…hapo ndipo akaniambia kuwa sitamaliza muhula huu…mimi nikamjibu kama haki itatendeka basi nitamaliza,” alisema.
Aliongeza kuwa baada ya kuhojiwa aliambiwa aondoke na kuwa wanafunzi wote ambao ni wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) lazima wataondolewa chuoni hapo.
“Ilipofika jana (juzi) ndipo alipokuja kiongozi wa bweni langu na kuniambia niende kuchukua barua yangu kwa mkuu wa kitivo changu…lakini cha ajabu vitu nilivyohojiwa hapo mwanzo tofauti na vilivyoandikwa kwenye hii barua ni tofauti,” alisema.
Naye, Rafiki Lufunga alisema: “Na mimi ni mmoja kati ya wanafunzi waliosimamishwa kisa, kuandamana hadi Utawala kwa ajili ya kudai haki yetu,” alisema.
Alisema sababu za kusimamishwa ni kuandamana hadi utawala kuulizia fedha zao za kujikimu ambazo hutolewa na Bodi ya Mikopo.
“Hivyo wote ambao tulikuwa tunauuliza uongozi maswali siku hiyo, tumepewa barua za kusimamishwa. Lakini nakwambia haki itabaki kuwa pale pale,” alisema.
Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Idris Kikula, alipotafutwa kuthibitisha hatua hiyo, simu yake ya mkononi haikupatikana na ile ya mezani iliita bila ya kupokelewa.
Hata ya Mkuu wa Chuo kitivo cha Elimu, Kabigumila haikupatikana.
Januari 3, mwaka huu wanafunzi zaidi ya 2,000 wa kitivo hicho waligoma kuushinikiza uongozi uwalipe fedha zao za kujikimu zinazotolewa na bodi ya mikopo.
Mgomo huo ulisitishwa baada ya uongozi wa chuo hicho kuwaahidi wanafunzi hao kuwalipa fedha hizo Januari 6, mwaka huu.
UDOM inavyosaidia kuikuza Dodoma
Wahenga walituasa kwa misemo mingi baadhi ni hii, ‘hakuna ubaya usio na uzuri ndani yake wala hakuna jema lisilo na kasoro.
Huo ndio ukweli kuhusu Dodoma, ina matatizo sugu ya maji, lakini ina maendeleo makubwa kielimu, kibiashara, kimajengo na kimaadili.
Mji wa Dodoma haujabadilika kihivyo, isipokuwa maisha yamepanda, vyakula, vyumba vya kuishi bei juu, kutokua haraka najua ni kwa sababu hayo ni maeneo ya kati ya mji.
Pembezoni mwa mji huo, mzunguko wa kilometa 10 hivi hali ni tofauti, mji unakua kwa kasi ya kutisha, nyumba bora na za kisasa zinaonekana hata miundombinu mingine, imeimarika.

Kasi ya kukua kwa mji wa Dodoma, si ile iliyodhaniwa na wengi waliodhani kusuasua kwa makao makuu kuhamia huko, na ujenzi wa taasisi kadha wa kadha kikiwamo Chuo Kikuu cha Dodoma, ungesuasua, kumbe si hivyo.
Udom, kwa wale wasiowahi kufika Dodoma siku za hivi karibuni, chuo kikuu hicho kimejengwa kifahari, kimantiki na kimaendeleo, kila kitivo, chuo au namna nyingine wanavyogawa wasomi, idara na migawanyo mingine mingi ya elimu, afya, mawasiliano, uongozi na mengine mengi, yamewekwa upande na upande mwa barabara za lami zinazozunguka kampasi hizo.
Majengo hayo hata ukiwa mbali, yanaonekana milimani upande wa kushoto mwa barabara ukitoka Dar es Salaam na kadiri unavyokaribia mjini ndivyo yanavyooneka vizuri na kwa mihimili yake iliyopanda juu.
Majengo hayo ni mengi, na kila ukipita barabarani , ukazunguka nyuma au mbele ya mlima, utakuta mejengo ama ya kitivo au ya uongozi na migawanyiko mingine.
Kwa Makisio yasiyo ya kitaalamu, inawezekana kabisa majengo ya chuo hicho yameshika eneo la kilometa 50, ni eneo kubwa ukweli huo ungebainika zaidi kama lingekuwa kwenye tambarare, lakini ni milimani.
Ukisogea karibu zaidi, ndipo unajua mtindo wa majengo hayo, yamepanda juu, yamejaa vioo na madoido mengine kadha wa kadha. Mtindo mpya ambao wabunifu, ama wachoraji na wote waliochangia kuyajenga majengo hayo wanastahili pongezi.
Januari Kilanzi, mkazi wa Kikuyu Dodoma anasema, tofauti na miaka michache iliyopita tuliyochoshwa na sera za makao makuu ya serikali kuhamia Dodoma tangu miaka 1970, sasa tunaamini kuwa tunachangamoto ya kuwekeza majengo kutokana na kuwapo chuo kikuu ambacho kinahitaji miundombinu mingi kutosheleza mahitaji ya wanafunzi, wakufunzi na watumishi wengine na taasisi nyingine.
Kutokana na uamuzi huo wa serikali kujenga chuo kikuu hicho, umeamsha ari ya wakazi wa Dodoma ambao sasa wamebadili mtazamo wao, sasa wanahaha kuwekeza kwenye majengo, hoteli, nyumba za wageni na majengo mengine kutosheleza mahitaji ya wakazi, wafanyakazi na wanafunzi watakaomwagika mjini hapo mara vitivo au chuo kikapofanya kazi kutosheleza uwezo wake.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Iyumbu, kilicho umbali mfupi kutoka chuoni, Yona Ngobito anasema kujengwa kwa Chuo Kikuu cha Dodoma, kimebadilisha mambo mengine na hivyo kuna changamoto nyingi zinatakiwa kutafutiwa ufumbuzi mapema.
Changamoto yao ni namna gani watalisha, wafadhili na kusaidia kulisha idadi kubwa ya watu ambao zaidi ya nusu laki wapo Udom peke yake, ukiachilia mbali katika taasisi nyingine za dini na serikali na nyinginezo.
Miaka michache iliyopita eneo ilipojengwa Udom, lilikuwa limeota misitu midogo, vichaka na sasa yamesimama majengo bora, majengo yenye hadhi na heshima ya chuo kikuu, kikubwa Dodoma, nchini na Afrika kwa ujumla.
UDOM, imechangia kuleta kasi ya maendeleo Dodoma, kwani lazima kwenda na kasi hiyo kwani lazima wanafunzi 40,000 na watumishi mamia kwa maelfu, watahitaji huduma muhimu zinazopatikana mjini Dodoma ili kukidhi haja na mahitaji yao ya kusoma au kufundisha chuoni na mahali pengine.
Kutokana na wingi wa wanafunzi hata watumishi, kuna changamoto kubwa inayowakabili wakazi wa Dodoma. Lakini pia ni changamoto kwa wawekezaji na wote wenye kujua umuhimu wa elimu nchini.
Hali ya majengo na miundombinu mingine, haijakaa kimtindo wa kupokea wanafunzi na wakufunzi wao zaidi ya nusu lakini wa Udom na wengine wa taasisi nyingine, haiwiani na mahitaji ya idadi ya watu wanaotakiwa wawepo mjini hapo na kutumia huduma hizo.
Changamoto hiyo ya uwekezaji si ya watu wa Dodoma pekee, nadhani ni ya Watanzania wote ambao kwa muda mrefu walijisahau kuwekeza katika sekta ya miundombinu wakidhani milango haijafunguliwa kumbe ipo wazi kuwekeza Dodoma na mahali pengine, ili kukidhi mahitaji ya majengo ya kutosha kwa ajili ya makazi, malazi na huduma nyingine kama hoteli, baa, nyumba za wageni na mengine kadha wa kadha.
Uwekezaji wa miundombinu mjini Dodoma hauhitaji subira, kinachotakiwa ni kuwasiliana na watu wa mipango miji, kujua wapi na namna gani viwanja vinapatikana ili kujenga miundombinu ya kuwasaidia wasomi na wafundishaji wapate mahali pa kuishi.
Matajiri na wote wenye malengo ya kuwekeza nchini, wajikite kuwekeza katika miundombinu ili isiibuke kero sugu ya usafiri kama ya jijini Dar es Salaam, kero ya usafiri kama vijijini ambako mbuzi, ng’ombe, paka, mbwa na wanyama wengine wanapanda gari moja na abiria.
Isije ikaibuka kero ya chakula kama vile Tanzania ipo jangwani, wakati nchi hii ina kila neema ya ardhi yenye rutuba na maji mengi yasiyotumiwa na mtu yeyote.
Changamoto ya miundombinu mjini Dodoma ni kama ya maji, kuna uhaba wa maji, kama yapo si ya kiwango kinachotakiwa, basi mamlaka husika na taasisi zinazoweza kuwekeza ziwekeze kwenye sekta hiyo, ili kuokoa wanafunzi watakaoenda kusoma hapo, wasiache masomo wakawa omba omba wa maji mitaani.
Kila mwenye uwezo wa kuwekeza na awekeze, Chuo Kikuu cha Dodoma kimefungua mipango kwa maana ya kwamba wanafunzi, walimu na watumishi pamoja na watu wengine watahitaji huduma mbalimbali ikiwamo miundombinu ambayo ni muhimu kuwapo ili kulingana na mahitaji ya sasa...